Sheria na Masharti

Kwa kutumia vipengele vya gumzo kutoka Google ("Huduma"), unakiri na kukubali kufuata Sheria na Masharti ya Google, Sera ya Faragha ya Google pamoja na masharti haya ya ziada (“Sheria na Masharti” kwa ujumla). Vipengele vya gumzo hufanya kazi pamoja na nambari za simu, kwa hivyo huenda vikapitia kwa watoa huduma wengine ili kufikia nambari hizo za simu. Unakubali kwamba anwani zako zinaweza kukaguliwa mara moja moja ili kuchunguza uwezo wa kutumia vipengele vya gumzo ili kutoa Huduma hii. Huenda Google ikabadilishana na mtoa huduma wako maelezo yako ya kifaa mara moja moja, vikiwemo vitambuzi vya kifaa au maelezo ya SIM kadi, ili kuthibitisha nambari yako ya simu na kukupa Huduma hii. Sheria na Masharti haya hayatumiki katika vipengele na huduma zinazotolewa na mtoa huduma wako (k.m., upigaji simu kupitia mtoa huduma za simu na utumaji ujumbe, zikiwemo huduma za SMS/MMS/n.k). Unaweza kuacha kutumia Huduma hii kwa kuizima kwenye mipangilio ya programu yako ya ujumbe.

Huduma hii inatolewa na Jibe Mobile, Inc., kampuni inayomilikiwa na Google LLC.