Sheria na Masharti ya gumzo la RCS

Kwa kutumia Gumzo la RCS kutoka Google, unakubali Sheria na Masharti ya Google, the Sera ya Faragha ya Google na masharti haya ya gumzo la RCS ("Sheria na Masharti" kwa ujumla). Gumzo la RCS hukuruhusu kutuma ujumbe kwa wengine kupitia nambari zao za simu, kwa hivyo ujumbe utapitia Google na wakati fulani, kupitia watoa huduma wengine (kama vile watoa huduma na programu nyingine za kutuma ujumbe) ili ufikie nambari hizo za simu. Unakubali kwamba kifaa chako na vifaa vya unaowasiliana nao vinaweza kukaguliwa nyakati fulani kuona uwezo wa RCS ili kuhakikisha kuwa unaweza kupokeza magumzo ya RCS. Mara moja moja, Google inaweza kubadilishana na mtoa huduma wako maelezo ya kifaa chako (vikiwemo vitambulishi vya kifaa au maelezo ya SIM kadi) ili kuthibitisha nambari yako ya simu (huenda ukatozwa ada za SMS) na kukupatia gumzo la RCS. Huenda ukatozwa gharama za data kwa sababu ya kutumia gumzo la RCS. Sheria na Masharti haya hayatumiki katika kipengele na huduma zozote zinazotolewa na mtoa huduma wako (kama vile upigaji simu kupitia mtoa huduma za simu na kutuma ujumbe, zikiwemo huduma za SMS na MMS). Unaweza kuacha kutumia gumzo la RCS kwa kuzima mipangilio hii kwenye Programu ya Messages kutoka Google.

Gumzo la RCS linatolewa na Jibe Mobile na unaingia katika mkataba na Jibe Mobile, Inc., inayopatikana 1600 Amphitheatre Parkway, Mountain View, CA 94043 Marekani. Ikiwa nambari yako ya msimbo wa nchi ni ya nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya au Uswisi, basi gumzo la RCS linatolewa na Jibe Mobile Limited, inayopatikana 70 Sir John Rogerson’s Quay, Dublin 2, Ayalandi na unaingia katika mkataba nayo ambapo Muhtasari huu wa Sheria na Masharti unatumika.